kiswahili Club

  

CHAMA CHA KISWAHILI CHA SHULE YA UPILI YA MARIAMUUANACHAMA
chama cha Kiswahili kina jumla ya wanachama hamsini na wawili.wanachama hawa ni wa kutoka madarasa mbalimbali.wanachama wa kidato cha nne ndio wengi,yaani kumi na wawili,kidato cha tatu  kumi na mmoja,kidato cha pili kumi na kidato cha kwanza,wanachama tisa.

MADHUMUNI

1. kukikuza na kukiendeleza Kiswahili katika jamii
2. kuimarisha masomo ya kiswahili
3. kuhakikisha ufanisi wa kiswahili
4. kuizindua jamii kuhusu maswala tofauti yanayoibuka,yanayoathiri lugha ya Kiswahili
5. kuhakikisha uzungumzaji wa lugha sanifu
6. kumaliza athari za lugha ya ‘sheng’ katika jamii
7. kusaidia kukuza na kuimarisha vipawa vya wanafunzi katika lugha ya Kiswahili kama vile ushairi na ulumbi

SHUGHULI ZA CHAMA
 1. chama hiki hushiriki katika baadhi ya kongamano za Kiswahili ambazo husaidia katika uchambuzi muhimu vya kiswahili
 2. mijadala pia huandaliwa na chama cha Kiswahili na huwa baina ya wanafunzi wa shule tofauti mara moja kwa muhula
 3. chama pia hanta siku ya kusherehekea utamaduni wa Kiswahili ambayo huwa muhula wa kwanza kila mwaka
 4. huzuru vyuo vilivyohitimu katika lugha hii na pia nyumba na vikao  vya utangazaji vilivyobobea katika upeperushaji wa ujumbe kwa   lugha sanifu ya kiswahili
 5. hanta malaria ya Kiswahili yanayowekwa katika maktaba ya shule
 6. hanta na kuwaalika watu mashuhuri waliohitimu katika masomo ya Kiswahili ili kuja kuwaelimisha wanafunzi na pia kuchambua vitabu vinavyohusika na fasihi.

UFANISI

1. chama hiki kimefanikiwa na kuweza kuzuru vituo kadhaa vya utangazaji wa lugha ya kiswahili
2. chama pia kimehitimu katika kuwaalika waandishi wa vitabu tofauti vya kiswahili na pia wanaosahihisha mitihani mikuu ya kitaifa
3. mwaka wa elfu mbili na tisa,tulizuru na kushiriki katika kongamao ya Kiswahili katika shule ya wasichana ya Naivasha
4. chama pia kimeshiriki katika uandishi wa majarida ya kiswahili yaliyowekwa kwenye maktaba
5. chama kimesaidia katika kukuza kwa lugha hii ya kiswahili kuitupilia mbali lugha ya ‘sheng’


VIONGOZI WA CHAMA

BWANA WAWERU
 1.      MWENYEKITI: CATHERINE NJOROGE.
 2.      NAIBU MWENYEKITI: JOYANN WAWERU.
 3.      MWEKAHAZINA: BEATRICE BWONDA.
 4.      KATIBU: DANIELLA LANG’AT
 5.      MWAKILISHI WA KIDATO CHA KWANZA: EVELYNE KEIS.
 6.      MWAKILISHI WA KIDATO CHA PILI: CATHERINE KEMUMA.
 7.      MWAKILISHI WA KIDATO CHA TATU: EURELLAH LAQUISHA.
 8.      MWAKILISHI WA KIDATO CHA NNE.
KIRANJA WA CHAMA: BWANA BENSON NGIGE

NEW ADMIN BLOCK

PICTURES OF OUR NEW ADMINISTRATION BLOCK(UNDER CONSTRUCTION)

              …

read more

TERM DATES

MARY MOUNT SECONDARY SCHOOL TERM DATES FOR TERM 2 2013

1.Click here to view term dates 

read more